Wasiliana nasi | MMM | Barua Pepe |

TAARIFA KWA UMMAKUHUSU UTARATIBU WA KUONA WAGONJWA WALIOLAZWA NA WAGENI

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya unaufahamisha umma kwamba kuanzia tarehe 17/04/2020 na kuendelea utaratibu utakua kama ifuatavyo;

Ndugu wa wagonjwa watakaokua wanakuja kuwaona ndugu waliolazwa kuhakikisha wana kadi ya kuingilia getini. Hivo endapo hutakua na kadi hautaruhusiwa kuingia getini.

Pia ndugu wa wagonjwa pamoja na wadau wote watakaofika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya kupata huduma watatakiwa kuandika majina na namba ya simu kwenye kitabu cha wageni kilichopo getini kwa walinzi.

Hatua hii inakuja ikiwa ni sehemu ya mkakati wa taasisi wa kuhakikisha wagonjwa, ndugu wa wagonjwa pamoja na wadau wetu wanakua salaama dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa corona (COVID-19).

Pia ni lazima kusafisha mikono kwa vitakasa mikono kila unapoingia na kutoka ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, Jikinge Wakinge Wengine.

Imetolewa na ;

 Kitengo Cha Mawasiliano Na Uhusiano

- 17 April 2020