Wasiliana nasi | MMM | Barua Pepe |

Historia

Hospitali ya Rufaa ya mkoa Mbeya inapatikana katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya mtaa wa Forest mpya.Ujenzi wa Hosptali hii ulianza rasmi mwaka 1988.Wazo na nia ya ujenzi wa Hospitali hii ulitokana na kuwepo kwa mlundikano(congestion) wa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya na Hospitali za wilaya kwa ujumla.

Ilianza kufanya kazi mwaka 1990 kama ofisi ya mkuu wa mkoa, na baadae mwaka 2002 ilianza kutoa huduma ya magonjwa ya nje(outpatient services).Mwaka 2010 mwezi wa kwanza hospitali ilianza kutoa huduma ya magonjwa ya ndani(inipatient services na baadae mpaka sasa huduma ya afya ya uzazi ikaanza kutolewa.Mpaka sasa hospitali inahudumia zaidi ya wakazi milioni 1.9 ndani na Nje ya jiji la Mbeya.

Hospitali ina vitanda 56 kwa idara ya magonjwa ya ndani,46 idara ya afya ya uzazi,62 idara ya watoto na kufanya hospitali nzima kuwa na jumla ya vitanda 180.Hospitali inategemea kuwa na jumla ya vitanda visivyopungua 365 mpaka kukamilika kwa ujenzi wa idara zote.