Social welfare Services
Kitengo cha Ustawi wa Jamii
	
Zifuatazo ni huduma zinazotolewa na kitengo cha Ustawi wa Jamii:
- Kufanya uchunguzi na kutoa msamaha kwa wagonjwa wasio na uwezo na wale walio kwenye makundi hatarishi
 - Kutoa ushauri wa kisaikolojia kwa wagonjwa/ndugu wa wagonjwa na watumishi wenye matatizo ya kijamii au kisaikolojia
 - Kuhudhuria kliniki ya uangalizi na matibabu ya UKIMWI (CTC) na kutoa ushauri kwa wagonjwa kwa wale watakaobainika kuwa na matatizo ya kijamii ambayo hupelekea kuwa wafuasi wazuri wa dawa
 - Kuhudhuria major ward rounds na social ward rounds ili kugundua wagonjwa watakaohitaji huduma ya ki ustawi
 - Kushuhulikia mashauri ya ukatili wa jinsia na ukatili dhidi ya watoto
 - Kushirikiana na vitengo vingine katika shuhuli za uchangiaji damu
 - Kuwaunganisha wagonjwa na vyanzo vingine vya huduma nje ya hospitali
 - Kuwaunganisha wagonjwa na familia zao
 - Kushuhulika na wagonjwa waliotelekezwa wakiwemo watoto wachanga
 - Kushuhulikia mashauri mengine ya kijamii kwa kadiri yatakavyoibuka
 - Kutoa elimu ya afya kwenye jamii kwaajili ya kuleta uelewa juu ya masuala mbalimbali yahusuyo afya
 - Kufanya supportive supervision kwa vituo vya afya
 
	
Muda wa huduma:
kuanzia saa 1:30 hadi saa 9:30 kila siku za kazi
	


