Afya ya jamii
Jifunze njia za kujikinga na maambukizi ya Ebola.
Njia za kujikinga na ugonjwa huu ni :
- Epuka kusalimiana kwa kushikana mikono au kukumbatiana
- Epuka kugusa damu, matapishi, mkojo, kinyesi, kamasi, mate, machozi na maji maji mengine yanayotoka mwilini mwa mtu mwenye dalili za ugonjwa huu
- Epuka kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyekufaakiwa na dalili za ebola badala yake toa taarifa kwa uongozi wa serikali ili wasimamie taatibu za mazishi
- Epuka kutumia nguo, shuka, blanketi, kitanda nagodoro za mtu aliyeambukizwa ugonjwa, toa taarifa kwenye ofisi za serikali ya eneo husika
- Kwa kuwa ugonjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, epuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja
- Nawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni mara unapomtembelea mgonjwa hospitalini au kumhudumia nyumbani
- Epuka kugusa wanyama kama vile popo, nyani, sokwe, tumbili na swala au mizoga ya wanyama
- Zingatia ushauri na maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya na viongozi wa serikali.
- Wahi kituo cha kutolea huduma za afya uonapo dalili za ugonjwa wa Ebola
- Toa taaifa mapema kwa watoa huduma za afya uonapo mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola au kifo
- Zingatia usafi binafsi pamoja na usafi wa mazingira yako.
HEDHI - CUP.