Kliniki ya Magonjwa ya ukimwi
Posted on: December 21st, 2024Hii ni kliniki inayohusika na kutibu wagonjwa wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na madhara yatokanayo na ugonjwa huo. Kliniki hii ipo kila siku kuanzia muda wa saa 3 asubuhi mpaka saa 9 na nusu mchana, pia kliniki ya jioni kuanzia saa 10 kamili jioni mpaka saa 2 kamili usiku. Pia kliniki ya watoto kila jumamosi na kliniki ya vijana mara moja kwa mwezi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.