Wasiliana nasi | MMM | Barua Pepe |

HABARI PICHA ZIKIONYESHA WANANCHI MBALIMBALI WALIOTEMBELEA KWENYE JENGO LA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MBEYA KWENYE MAONYESHO YA NANENANE.

Posted on: August 1st, 2023


Wananchi wamefurahishwa na jinsi Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa mbeya walivyo jipanga katika kutoa elimu na kuwajulisha wananchi huduma mbalimbali zinazotilewa katika idara mbalimbali za Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa mbeya. Hata hivyo furaha kubwa kwa wananchii ni kuona jinsi huduma zilivyoboreshwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa mbeya tofauti kubwa na miaka ya nyuma, sasa huduma Bobezi ni za uhakika na kuongezeka kwa huduma za kiuchunguzi nazo zilikuwa kivutio kikubwa kwa kila mwananchi aliefika katika Jengo la Hospitali ya  rufaa ya mkoa wa Mbeya.

 Aidha, kilichowavutia zaidi ni ukarimu wa watoa huduma na uwezo wa kuelezea kwa ufasaha huduma zinazopatikana katika idara zao na Hospitali kwa ujumla. Huku wananchi wakifurahishwa na kuona sasa ndio kimbilio lao katika matibabu ya magonjwa mbalimbali kutokana na uboreshaji wa huduma na uwepo wa Madaktari bingwa mbalimbali Hospitali ya rufaa ya mkoa mbeya