Wasiliana nasi | MMM | Barua Pepe |

JINSI YA KUPIGA MENO YAKO VIZURI

Posted on: March 18th, 2024

Daktari Nyoni wa Kinywa na Meno habari katika picha, katika muendelezo wa kuendelea kutoa elimu juu ya afya ya kinywa na meno leo tarehe 18 machi,2024 ilikuwa zamu ya shule ya wasichana ya Loleza kutoa elimu "Jinsi ya kupiga mswaki meno yako vizuri"

Kupiga mswaki vizuri kutaweka meno na ufizi wako katika afya nzuri na kupunguza hatari ya kupata magonjwa sugu.Lakini wengi wetu hatupigi mswaki ipasavyo.

Tumekuwa tukipiga mswaki tangu tukiwa wadodgo, wafupi kuliko vioo vya kawaida vya bafuni. Lakini wachache wetu wanajua jinsi ya kupiga mswaki meno vizuri.

Walakini, kuna habari nyingi juu ya jinsi ya kusugua meno yako vizuri. Kwa hiyo inaweza kuwa na utata zaidi. Kulingana na utafiti mmoja, kuna habari nyingi zinazokinzana kati ya ushauri wa wataalam wa kupiga mswaki.

Nigel Carter, mtaalamu wa Afya ya Kinywa nchini Uingereza, alisema: "Kuna aina nyingi tofauti za habari ambazo zinakinzana na zinachanganya zaidi kwa watumiaji." Kuchanganyikiwa kunachochewa zaidi na bidhaa zinazotolewa kwa ajili ya afya ya meno, kama vile visafisha ulimi na dawa za kusukutua za maji.

Kwa hivyo unakosea wapi wakat wa kupiga mswaki? Na unasafishaje ipasavyo?

Njia bora

"Wagonjwa wengi wa meno wanajua wanahitaji kuondoa uchafu wa chakula," Hersheyfield alisema. "Lakini hiyo ni nusu ya ukweli. Kuondoa bakteria kwenye meno yako ni muhimu zaidi."

Bakteria na vijidudu wanaoishi katika kinywa cha kila mtu huunda biofilm nene (utando nyembamba ulio na bakteria au vijidudu) unayoitwa plaque. Plaque ina takriban aina 700 za bakteria na kuifanya kuwa mahali pa kuzaliana kwa fangasi na virusi. "utando huo wa kunata kwenye meno na tishu laini hautoki kwa urahisi, kwa hivyo inapaswa kusafishwa kwa njia ya bandia," Nyoni alisema.

Eneo muhimu zaidi la kuondoa plaque ni kwenye mstari wa ufizi na sio meno. Vijidudu vidogo (Microorganisms) hupenya katika tishu za ufizi kupitia eneo hili na kusababisha kuvimba na hatimaye ugonjwa wa periodontitis