Wasiliana nasi | MMM | Barua Pepe |

Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Ngwilo Mwakyusa amewaongoza watumishi kuaga mwili wa mtumishi Agnes Mgani

Posted on: August 16th, 2022

Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Ngwilo Mwakyusa amewaongoza watumishi kuaga mwili wa Agnes Victory Mgani ambaye alikuwa mtumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya kwenye viwanja vya Hospitali . 


Aidha, Kaimu Mganga Mfawidhi ametoa Pole kwa Watumishi na ndugu wa marehemu kwa niaba ya Bodi ya Ushauri na menejimenti ya Hospitali. 


Hata hivo Kaimu Mganga Mfawidhi Amewaomba watumishi kuendelea kuiombea Familia ya Mgani katika kipindi hiki cha kumpoteza mpendwa wao.


Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe!