Mafanikio yaliyopatikana katika hospitali ya mkoa wa mbeya kwa miaka minne ya serikali ya awamu ya tano.
Posted on: December 23rd, 2019- Upatikanaji wa dawa katika hospitali ya Rufaa mkoa wa mbeya sasa ni asilimia 95%
- Tumeboresha huduma mbalimbali za uchunguzi ikiwemo za Radiolojia na maabara ,katika kipindi hiki cha miaka minne vipimo vyote vinapatikana katika hospitali ya Rufaa mkoa wa mbeya.
- Tumeanzisha kliniki za kibingwa katika hospitali yetu hatua iliyochangia kuimarisha huduma ya mama na mtoto,kwa mwezi tunahudumia takribani kina mama 600
- Tunatumia mfumo wa kielektroniki katika kukusanya mapato ya hospitali kwa sasa tunakusanya Tsh. Milioni 100 kutoka milioni 40 kwa mwezi ikiwa ni keshi. Fedha hizi zinasaidia kuboresha huduma ikiwemo kununua dawa.