MAKABIDHIANO YA OFISI NAIBU WAZIRI WA AFYA
Posted on: May 21st, 2020Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wazee na Watoto Mhe. Godwin Ole Mollel amewasili katika Ofisi za Wizara ya Afya zilizoko Mtumba Jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ikulu ya Chamwino mapema leo. Dr. Mollel amekabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Dkt. Faustine Ndugulile huku Waziri Ummy Mwalimu akishuhudia makabidhiano hayo. Naibu Waziri aliyepita Dkt. Faustine Ndugulile amemshukuru Waziri pamoja na Wafanyakazi wote wa wizara ya Afya kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote alichotumikia Wizara hii. #KaribuDkt.Mollel #Kwaheri @faustine_ndugulile