Wasiliana nasi | MMM | Barua Pepe |

Mganga Mfawidhi Dkt Abdallah Mmbaga amefanya kikao na watumishi Idara ya Maabara

Posted on: August 31st, 2022

Mganga Mfawidhi Dkt Abdallah Mmbaga (wa pili kutoka kulia) amefanya kikao na Watumishi wa Idara ya Maabara kwa lengo la kusikiliza changamoto na maoni ya Idara ili kuboresha Huduma.


Aidha, Mganga Mfawidhi Dkt Abdallah Mmbaga pamoja na mambo mengine, ametoa wito kwa Wataalamu wa Maabara kuhakikisha huduma bora kwa wananchi zinatolewa pasipo na vikwazo vyovyote. 


Hata hivo akisisitiza juu ya Umuhimu wa kila Mtumishi kuwajibika katika kuwahudumia Wananchi, amesema hakuna sababu ya kutokutolewa huduma bora kwa sababu Maabara ni ya kisasa na ina viyendea kazi vya kisasa.