Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Salum Manyata ametembelea Banda la Hospitali ya Rufaa ya
Posted on: August 4th, 2022Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Salum Manyata ametembelea Banda la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale Nanenane ili kuona huduma zinazotolewa kwenye Banda la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mbeya.
Aidha Mganga Mkuu, akiwa ametembelea Banda la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya amempongeza Mganga Mfawidhi Dkt Abdallah Mmbaga kwa ubunifu wa kushiriki kwenye maonesho ya nanenane ambapo amesema kupitia maonesho ya nanenane itasaidia wananchi kufahamu huduma zinazotolewa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
Hata hivo Mganga Mkuu Dkt Salum Manyata ameshiriki kuhamasisha wananchi kufika kwenye Banda la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya kupata Elimu juu ya huduma zinazopatikana Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya kutokana na uwekezaji mkubwa wa serikali ya awamu ya sita, ambapo sasa Huduma za upasuaji na Huduma za dharura zimeongezeka sambamba na uboreshaji wa Vifaa vya kiuchunguzi.