Wasiliana nasi | MMM | Barua Pepe |

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera amefanya ziara hospitali ya rufaa ya mkoa na kufanya kikao na watumishi kuhusu uboreshaji wa Huduma

Posted on: April 24th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera akiambatana na Katibu Tawala wa mkoa Dkt. Angelina Lutambi, wamefanya kikao na wakuu wa Idara na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya. 


Mhe. Mkuu wa mkoa amewapongeza watumishi kwa kuendelea kutoa huduma kwa Wananchi, zaidi ameagiza kufanyike maboresho katika utoaji wa huduma ili kujenga Imani kwa wananchi kuendelea kuona Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya iwe kimbilio kwa kila mwananchi tofauti na mitazamo iliyopo sasa.


Aidha, mkuu wa mkoa ameagiza kuhakikisha Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya inawapa kipaumbele wazee wanapofika kupata huduma maana katika kuwahudumia wazee ni baraka. Hivyo ameagiza kuendelea na utaratibu wa kuwatengea dirisha maalumu la wazee ili kupunguza usumbufu.


Hata hivo, mkuu wa mkoa ameagiza ndani ya mwezi mmoja Hospitali iwe imeanzisha Duka la dawa ili kuhakikisha dawa zote zinapatikana kuondoa usumbufu wa wagonjwa kukosa badhi ya dawa.


Mkuu wa mkoa amesema ataendelea kufatilia kwa karibu utekelezaji wa maagizo yote aliyotoa, zaidi akisisitiza huduma bora kwa wateja iwe kipaumbele cha kila wakati.