Wasiliana nasi | MMM | Barua Pepe |

Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Julius Kaijage ameongoza kikao cha Bodi na kutembelea miradi inayoendelea

Posted on: May 18th, 2022

Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri amewaongoza wajumbe wa Bodi kukagua utekelezaji wa miradi  inayoendelea. Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na wajumbe wa Bodi ni mradi wa ujenzi wa jengo la Upasuaji, ICU, Nyumba ya mtumishi, na Jengo la dharura.


Wajumbe wamefurahishwa na utekelezaji ambao unaendelea kwenye miradi mikubwa ya Jengo la Upasuaji na Dharura.


Aidha , Mwenyekiti wa bodi pamoja na wajumbe wameelekeza kuongeza kasi zaidi ili kuweza kuboresha huduma kwa wananchi.


Hata hivyo, baada ya kutembelea miradi inayotekelezwa Mawenyekiti aliongoza kikao cha Bodi ya Hospitali ikiwa ni kikao cha kiutendaji kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa.