Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ametembelea Banda la Hospitali kwenye Maonyesho ya Nanenane
Posted on: August 4th, 2022Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya Dkt. Julius Kaijage, ametembelea Banda la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya kuona huduma zinazotolewa.
Aidha, Dkt Kaijage ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri amepongeza kwa huduma zinazotolewa kwa wananchi, pia amefurahishwa na jinsi Taasisi inavojitangaza kwa Umma ambapo inasaidia wananchi kutambua aina ya Huduma zinazopatikana Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
Mwisho ameahidi kupitia maonyesho ya mwaka huu iwe chachu ya kufanya maandalizi zaidi kwa maonyesho ya Nanenane mwakani.