Wiki ya Afya ya KInywa na Meno
Posted on: March 15th, 2024Daktari Geophrey Nyoni akiwaelezea wanafunzi wa Chuo cha Kilimo -Uyole Jinsi ya kupiga mswaki meno, ikiwa ni mwendelezo wa kutoa Elimu juu ya Afya ya Kinywa na Meno katika wiki ya Afya ya Kinywa na Meno.
Daktari Nyoni amewaeleza hatua za kufuata wakati wa kupiga mswaki meno;
1.Piga mswaki mara mbili kwa siku na mswaki laini na dawa ya meno yenye floraidi. Tema mate usisuuze.
2.Anza kwa kushika mswaki kando
kwenye pembe ya digrii 45 ambapo
ufizi na meno yanakutana.
3.Hakisha ufumwele uguse yote jino na ufizi.
4Tumia mwendo wa mviringo wa
upole ili kupiga mswaki nyuso zote
za kila jino.
5.Nyuso za nje Tumia karibu sekundi 10 na kila jino kabla ya kusogeza kwenye jino lijalo.
6.Rudia hadi meno yote ya juu na ya chini ni safi.
7.Nyuso za kuuma Papaswa nyuma na nje ili kusafisha meno ya juu na ya chini.
8.Piga mswaki ulimi Piga mswaki kuanzia nyuma kuja mbele ili kuondoa ukoga, unaosababisha pumzi mbaya.