Wasiliana nasi | MMM | Barua Pepe |

Ziara ya Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima kutembelea Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya

Posted on: March 10th, 2021

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe.Dkt Dorothy Gwajima amefanya ziara ya kikazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya (Mbeya RRH), Lengo ikiwa ni kuangalia utoaji wa Huduma kwa Wananchi na kutembelea miradi inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya awamu ya Tano. 


 Mhe. Dkt Dorothy Gwajima ametembelea ujenzi wa jengo la upasuaji (Surgical)na Jengo la dharura (EMD) ambapo amepongeza Uongozi wa Mkoa na Hospitali kwa usimamizi wa miradi mikubwa ambayo Serikali imetoa pesa ili kuboresha huduma za Afya kwa Wananchi wanyonge.