IJUE HOMA YA INI
Posted on: September 28th, 2019Ni ugonjwa unaosababishwa na virus aina ya hepatotrophic /hepatitis ambavyo hushambulia ini . virus ivyo hushambulia ini ambavyo vimegawanyika katika makundi 5 yaani A, B, C,D na E
HOMA YA INI INAYOSABABISHWA NA VIRUS VYA KUNDI A NA E
Huenezwa kwa njia ya kunywa maji au kula chakula kilicho chafuliwa au kushambuliwa na vijidudu vya kinyesi
Virus hivi hushambulia ini na kusababisha homa kali inayoambatana na dalili nyingne
KIRUSI E
Kirusi E kinaweza kusababisha mlipuko , hata ivyo ugonjwa unaosabishwa na virus vya A na E hupona baada ya miezi 2 mpaka miezi 3
NJIA ZA KUJIKINGA NA VIRUS VYA AINA A na E
Kuzingatia kanuni bora za Afya yaani unyonywaji wa maji safi na salama , ulaji wa chakula safi na matumizi bora ya choo kwa bahati nzuri virus vya A na E siyo tishio kubwa sana katika afya jamii
HOMA YA INI INAYOSABABISHWA NA VIRUS VYA KUNDI B ,C NA D
Huambukizwa kwa njia njia ya kuongezewa damu yenye virus vya ugonjwa huo, kujidunga sindano yenye virus vya ugonjwa huo , kushika maji maji kama vile matapishi , jasho kama mtu ana kidonda
Njia nyingne kubwa ya kuambukiza virus vya homa ya kundi B ni kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua au kipindi cha ujauzito
Virus vya hepatitis B vinaweza kukaa nje ya mwili wa binadamu kwa muda ya siku 7 na kuweza kusababisha maambukizi pale vitakapoingia ndani ya mwili wa binadamu ambaye hajapata kinga
MUDA WA KUONESHA DALILI ( INCUBATION PERIOD)
Kwa wastani uchukua muda wa siku 75 toka mtu apate maambukizi hadi aoneshe dalili
Virus vya kundi B na C vinapoingia ndani ya mwili wa binadamu hushambulia ini na kuweza kusababisha uambukizi sugu na wa muda mrefu na baadhi yao hupelekea ini kusinyaa ( Cirrhosis ) na pengine kupelekea kupata saratani ya ini
Virus vya kundi D mara nyingi humpata mtu mwenye alieambukizwa virusi vya kundi B ( co –infection)
TWAKWIMU
Ugonjwa wa Homa ya ini ya kundi B ( Hepatitis B) ndio unaongoza hapa nchini Tanzania kwa idadi kubwa ya ambapo utafiti wa mwaka 2017 uliofanywa kwa wachangiaji damu 233,953 , 4.9% (11,417) iligundulika kuwa na maambukizi ya homa ya ini ya B ( hepatitis B )