Wasiliana nasi | MMM | Barua Pepe |

Huduma ya Wagonjwa wa Nje

Posted on: January 5th, 2025

HUDUMA ZITOLEWAZO KATIKA KITENGO CHA WAGONJWA WA NJE HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MBEYA

Katika idara ya wagonjwa wa nje tunahudumia wastani wa wateja 250 kwa siku. Tuna idadi ya kutosha ya wafanyakazi ikiwemo madaktari na wauguzi kwa kutoa huduma bora zinastohili kila siku. Ifuatayo ni orodha ya huduma zinazotolewa katika idara yetu ya wagonjwa wa nje.

  • Tunatoa huduma za kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo ya dharula masaa 24
  • Tunatoa huduma za kiafya kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia kama vile kubakwa kila siku
  • Tunatoa huduma za uchunguzi wa afya kwa makundi mbalimbali kama wanafunzi na watu wengine wanaohitaji huduma kama hii kila siku.
  • Tunatoa huduma ya USHAURI NASAHA na upimaji wa VIRUSI VYA UKIMWI (VVU) bure kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa
  • Tunatoa huduma ndogondogo za upasuaji kama vile kushona majeraha, kusafisha vidonda, na kuhudumia waliovunjika kila siku.

  •                         ASANTE KWA KUTUCHAGUA TUKUHUDUMIE
  •                                                                                                                                                                              Daktari Greater akitoa huduma kwa mgonjwa kwa kutumia mfumo wa kieletroniki.